Serikali ya Sudan Kusini imekataa kata kata pendekezo la viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki la kuongeza wanajeshi zaidi wa kulinda amani nchini humo.
Mkutano wa mataifa ya muungano wa Afrika unaoendelea huko Kigali Rwanda unatarajwa kujadili kwa kina swala la mizozo ya Burundi na Sudan kusini miongoni mwa mengineyo.
Serikali ya Rwanda imepuzilia mbali ombi la mahakama ya kimataifa ya jinai yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi ICC ya kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir.
Jumuiya ya waislamu nchini Rwanda iliafikia uamuzi wa kuipiga marufuku vazi hilo la Niqab linalovaliwa na wanawake waislamu kutokana na kuibuka kwa visa vya utovu wa usalama unaosingiziwa kwa watu waliovalia Niqab